Na mwandishi wetu
Wachezaji 13 wa mchezo wa Judo wameanza kambi Ukonga, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afrika ya All African Game itakayofanyika nchini Ghana, mwakani.
Katibu Mkuu wa Judo, Innocent Mallya amesema leo Alhamisi kuwa wameona waanze kujiimarisha katika kambi ya kwenda na kurudi huku wakisubiri kambi rasmi yenye maelekezo ya Serikali siku za usoni.
Alisema msimu huu wamedhamiria kurudi na medali ndio maana wameanza mapema maandalizi ya kujiimarisha.
“Hatutaki kwenda kushiriki bali kushindana na kurudi na medali, timu yetu imeshaanza mazoezi katika kambi iliyoko Ukonga Magereza, naamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Mallya.
Mallya alisema wachezaji walioingia kambini kwa sasa ni wale wenye uzoefu katika mashindano ya kimataifa na wengine wamechaguliwa kutokana na mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Katibu huyo aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuisapoti timu hiyo ili iweze kukaa katika mazingira mazuri ya kambi na kujiandaa kwa utulivu.
Sports Mix Judo waanza maandalizi All Africa Games
Judo waanza maandalizi All Africa Games
Read also