Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba amefanya mazungumzo yenye mwelekeo mzuri katika kikao chake na wawekezaji wapya wa klabu hiyo, kampuni ya Ineos inayomilikiwa na bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe.
Ten Hag alikutana na Ratcliffe Jumanne iliyopita kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu bilionea huyo anunue asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo wakati wa Krismasi.
Akizungumzia kikao hicho, Ten Hag alisema alitumua muda mwingi na Ratcliffe pamoja na Sir Dave Brailsford na John-Claude Blanc ambao pia ni wawakilishi wa kampuni ya Ineos.
“Yalikuwa mazungumzo yenye mwelekeo mzuri, kilikuwa kikao kirefu kilichotumia saa kadha, tulikaa pamoja na kujadili ishu mbalimbali na tulikuwa katika mtazamo sahihi, kilikuwa ni kikao cha kujenga na tunaangalia namna ya kufanya kazi pamoja,” alisema Ten Hag.
Mabosi wa Ineos wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa klabu hiyo ingawa kuna kanuni za soko la hisa zinazowakataza kufanya jambo hilo kwa wakati huu.
Ten Hag hata hivyo alisema bado ni mapema mno kufanya mambo makubwa hasa kwa kuwa Ratcliffe na washirika wake ndio kwanza wamewasili Jumanne na kutumia muda wao mwingi katika klabu hiyo.
Alisema kwamba bilionea huyo na washirika wake walifika katika klabu hiyo pamoja na mambo mengine kwa ajili ya kuwajua maofisa wa klabu na kujua taratibu za uendeshaji wa klabu zilivyo.
Kimataifa Ten Hag, bilionea mpya wateta
Ten Hag, bilionea mpya wateta
Read also