Paris, Ufaransa
Straika Olivier Giroud ameweka rekodi ya kuifungia bao timu ya Taifa ya Ufaransa au Les Bleus akiwa na umri mkubwa wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Austria katika mechi ya Uefa Nations Ligi.
Giroud amefunga bao hilo jana akiwa na miaka 35 na siku 357 na anakuwa amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Roger Marche ambaye Desemba 1959 pia aliifungia Ufaransa bao katika mechi dhidi ya Hispania naye akiwa na miaka 35 lakini mdogo siku 70 kwa Giroud.
Ufaransa ilianza kulisakama mapema lango la Austria na Kylian Mbappe alipata bao lakini mwamuzi alilikataa kwa kuwa mfungaji aliotea, baadaye Aurelien Tchouameni alitaka kufunga goli la tikitaka lakini mpira alioupiga haukuzaa bao.
Kasi ya Ufaransa kusaka bao hatimaye ilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 56 baada ya Giroud kumuunganishia pande Mbappe ambaye aliwahadaa mabeki kadhaa wa Austria kabla ya kuujaza mpira wavuni kwa shuti la umbali wa mita 16.
Giroud alikamilisha bao la pili na la ushindi kwa timu hiyo katika dakika ya 65 akiujaza wavuni mpira kwa kichwa na kuipa Ufaransa ushindi muhimu ambao kama ingeukosa ingekuwa imejiweka pabaya katika michuano hiyo.
Kwa Giroud mbali na bao hilo kumfanya avunje rekodi ya kufunga bao akiwa na umri mkubwa, pia linamsogeza katika kuifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Thierry Hnery ambaye ameifungia Ufaransa mabao 51 wakati Giroud hadi sasa ana mabao 49.
Matokeo ya mechi za jana za Uefa Nations Ligi ni kama ifuatavyo
Ufaransa 2-0 Austria
Ubelgiji 2-1 Wales
Poland 0- 2 Uholanzi
Kazakhstan 2-1 Belarus
Latvia 1-2 Moldova
Croatia 2-1 Denmark
Slovakia 1-2 Azerbaijan
Liechtenstein 0-2 Andorra
Lithuania 1-1 Faroe Islands
Turkey 3-3 Luxembourg
Kimataifa Giroud apiga bao la rekodi Ufaransa
Giroud apiga bao la rekodi Ufaransa
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
