Barcelona, Hispania 7
Kiungo wa Barcelona, Pedri amesema kama angekuwa na uwezo wa kusajili mchezaji yeyote duniani katika klabu hiyo basi ndoto yake ingekuwa kumsajili mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland.
Pedri ametoa kauli hiyo huku ikikumbukwa kwamba Rais wa Barcelona, Joan Laporta aliwahi kufanya mazungumzo na aliyekuwa wakala wa Haaland, marehemu Mino Raiola lakini mwishowe mchezaji huyo alisaini Man City mwaka 2022.
Haaland, 23, hadi sasa ameifungia Man City mabao 71 katika mechi 75 za timu hiyo na aliiwezesha kubeba mataji matatu (treble) msimu uliopita ya Ligi Kuu England (EPL), FA pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Jamaa ni balaa, anafunga mabao mengi,” alisema Pedri alipoulizwa mchezaji gani angependa amsajili Barca.
Barca kwa sasa mshambuliaji wake tishio ni Roberto Lewandowski, 35 ambaye tayari amepata mshindani wa namba baada ya timu hiyo kumsajili mshambuliaji Mbrazili, Vitor Roque kutoka klabu ya Athletico Paranaense.
Roque, 18 alijiunga na Barca wiki iliyopita na huenda kesho Alhamisi akawa uwanjani kuiwakilisha timu yake hiyo mpya ambayo itaumana na Las Palmas kama atakamilisha taratibu zote za La Liga.
Pedri pia alimsifia Roque akisema kwamba ni mchezaji mwenye kujiamini na bado kijana hivyo ana nafasi ya kuichezea Barca kwa kipindi kirefu.
“Wakati wote huwa ni mwenye kutabasamu, Wabrazili wana maajabu yao, jamaa bado kijana kwa hiyo tuache kumuuliza kama yeye ni Pele mpya lakini ni mchezaji mwenye kujiamini mno,” alisema Pedri.
Kimataifa Pedri amtamani Haaland Barca
Pedri amtamani Haaland Barca
Read also
