Barcelona, Hispania
Klabu za Barcelona na Chelsea zinatajwa kuwa na mkakati wa kubadili makocha kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu hizo huku Mikel Arteta wa Arsenal na Thomas Tuchel wa Bayern Munich wakianza kutajwa.
Kwa upande wa Barca tayari kocha wa timu hiyo, Xavi ametangaza kuondoka baada ya msimu huu na jina lililoibuka na kuwa juu ya mengine ni la kocha wa Arsenal, Arteta.
Chelsea nao wanadaiwa kuwa na mpango huo, kocha Mario Pochettino inadaiwa huenda akatimuliwa wakati wowote baada ya msimu huu na mpango wa timu hiyo ni kumrudisha kocha wao wa zamani Thomas Tuchel.
Tuchel (pichani juu) ambaye ana rekodi ya kuvutia Chelsea baada ya kuiwezesha kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutimuliwa, amekuwa na msimu wa hovyo Bayern Munich na tayari klabu hiyo imekubaliana na kocha huyo kuachana baada ya msimu huu.
Chelsea ambayo imefanya uwekezaji mkubwa inaona Pochettino ameshindwa kuendana na uwekezaji huo hivyo mabadiliko ni jambo lisiloepukika na mtu ambaye wamemfikiria kuchukua nafasi hiyo ni Tuchel.
Barca nayo licha ya Xavi kuiwezesha kubeba taji la La Liga msimu uliopita na ingawa timu hiyo inaendelea na mbio hizo msimu huu, kocha huyo amewahi kulalamika juhudi zake kutothaminiwa na mabosi wa klabu hiyo na ndio maana akatangaza kujiweka kando baada ya msumu huu.
Arsenal pia imekuwa na mwenendo mzuri kwenye Ligi Kuu England (EPL) msimu huu na hata msimu uliopita lakini imeendelea kuwa na tatizo la kuyumba mwishoni mwa msimu jambo ambalo huenda likamshawishi Arteta kuwa tayari kwenda Barca kupata changamoto mpya.
Kimataifa Tuchel atajwa Chelsea, Arteta Barca
Tuchel atajwa Chelsea, Arteta Barca
Read also