Na mwandishi wetu
Winga mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema amejiunga na timu hiyo kwa lengo la kucheza na siyo kukaa benchi.
Chasambi ameyazungumza hayo muda mchache baada ya kutambulishwa rasmi na timu hiyo Jumatatu, akifafanua kuwa ingawa timu hiyo ina wachezaji wengi mahiri lakini atapambana kumshawishi kocha Abdelhak Benchikha kumpa nafasi.
“Najua ukubwa wa timu niliyojiunga nayo na changamoto ya nafasi lakini hilo kwangu si tatizo, nitapambana kuhakikisha nacheza kikosi cha kwanza lakini uwepo wa changamoto ni jambo zuri kwangu sababu itafanya niongeze bidii mazoezini,” alisema Chasambi.
Winga huyo alisema pamoja na kipaji alichonacho lakini bado ana mengi ya kujifunza kutoka kwa wachezaji wakongwe aliowakuta Simba na yupo tayari kwa ushirikiano ili kutimiza ndoto zake.
Alisema atahakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi ili kuipigania timu yao kufikia malengo ambayo wamekusudia kuyafikia mwishoni mwa msimu huu.
Chasambi ambaye ni mzawa amekuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa Simba kwenye dirisha dogo baada ya Salehe Karabaka na Babacar Sarr raia wa Senegal
Soka Chasambi halitaki benchi Simba
Chasambi halitaki benchi Simba
Related posts
Read also