Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Ligi Kuu NBC inatarajia kuendelea wakati wowote kuanzia sasa baada ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutolewa kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo (pichani) akieleza kwamba hiyo inatokana na kanuni kuruhusu ligi kuendelea.
“Kanuni inasema klabu yenye wachezaji wasiopungua watatu kwenye timu ya taifa basi michezo ya klabu hiyo itasimama, kwa sasa timu imetolewa kwenye mashindano ya Afcon, ni wazi kila klabu iliyokuwa na mchezaji wake kwenye timu ya taifa atakuwa amerudi kwa ajili ya mwendelezo wa ligi,” alisema Kasongo.
Kasongo alisema kabla ya fainali za Afcon kuanza, alieleza kuhusu kusimama kwa ligi na itarejea pale ambapo timu itakaporejea rasmi kutoka kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast.
Kasongo alisema baada ya hilo kueleweka Bodi inatarajia kukaa kufanya majumuisho na baadaye watatangaza rasmi tarehe ya kurudi kwa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Hadi ligi inasimama baadhi ya timu zilibakiza mechi moja kumaliza mzunguko wa kwanza huku nyingine zikiwemo klabu za Simba na Yanga zikibakiwa na michezo minne mpaka mitano huku Azam FC ikiwa kileleni mwa msimamo ikikusanya pointi 31.
Soka Pazia Ligi Kuu NBC kufunguliwa
Pazia Ligi Kuu NBC kufunguliwa
Read also