Na mwandishi wetu
Kuelekea mchezo wao wa keshokutwa wa raundi ya pili ya Kombe la FA, Azam imeahidi kuingia uwanjani kwa tahadhari na kuiheshimu Malimao FC ili kuhakikisha wanapata matokeo stahiki.
Kocha wa Azam, Kali Ongalla amesema licha ya ushindi wa mechi nane mfululizo kwenye Ligi Kuu NBC lakini bado wanahitaji kuwaheshimu wapinzani wao na watawakabili kiushindani ili kuendeleza ushindi kwenye kila michuano.
Malimao kutoka Katavi itavaana na Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam baada ya kufanikiwa kuiondosha City Gold kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
“Mechi ni mechi na hii ni michuano, hata kama tunaocheza nao hawana jina kubwa na sisi tuna rekodi nzuri hiyo haimaanishi kushusha ugumu wa mchezo, hii ni michuano tunahitaji ushindi na lazima tuwe na tahadhari ili kuhakikisha tunapata matokeo,” alisema Ongalla.
Ongalla pia amesema kwamba kwa sasa wapo kwenye maandalizi makali kwa ajili ya mechi hiyo na kikosi kinaonesha kipo vizuri na tayari kwa mapambano.
Soka Azam kuikabili Malimao FC kwa tahadhari
Azam kuikabili Malimao FC kwa tahadhari
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
