Na mwandishi wetu
Wakati kwa timu nyingine mastaa bado wako mapumzikoni kipindi hiki cha kupisha kalenda ya Fifa, huko Jangwani kocha Mtunisia Nasreddine Nabi hataki kusikia kitu kama hicho cha wachezaji kujiachia muda mrefu akihofia kushuka viwango hivyo kuwaita kambini fasta.
Hayo yanakuja wakati wenzao Simba wakitoa wiki mbili wachezaji kwa wake kupumzika wakati huu wa likizo lakini kwa Nabi yeye alitoa siku nne tu ambazo zimeisha jana Jumatano na leo Alhamisi wachezaji wote wanapaswa kuripoti kambini huko Avic Town, wilayani Kigamboni.
Meneja wa kikosi, Hafidh Saleh amethibitisha hilo. “Baada ya mchezo wetu wa FA dhidi ya Simba, tulitoa siku nne za mapumziko kisha tungerejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo unaofuata wa Ligi Kuu, dhidi ya Coastal Union.”
Hata hivyo wakati wanaanza mazoezi leo, kikosi chake kitakuwa bila mastaa 14; ambako 11 kati ya hao wako katika majukumu ya timu zao za taifa na watatu bado wanauguza majeraha.
Nane wako Taifa Stars; Aboutwalib Mshery, Bakari Nondo, Dickson Job, Farid Musa, Kibwana Shomari, Zawadi Mauya, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ na Feisal Salum. Wengine ni Mganda Khalid Aucho, Mkongomani, Shaban Djuma na kipa mdaka mishale Djigui Diarra wa Mali.
Soka Wachezaji Yanga kambini fasta
Wachezaji Yanga kambini fasta
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
