Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa lvory Coast, Adjé Silas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Ijumaa, katika mazungumzo yao viongozi hao, pamoja na kujadili kuhusu ushirikiano wa nchi hizo kwenye sekta ya michezo pia Ndumbaro amemualika Silas kushuhudia mechi ya Yanga dhidi ya Simba itakayochezwa Aprili 20, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mwaliko huo ni kwa ajili ya waziri huyo kushuhudia ladha ya mechi hiyo kubwa Afrika Mashariki pamoja na kuwaona wachezaji nyota wa timu hizo akiwemo Pacome Zouzoua, wa Yanga ambaye ni raia wa lvory Coast.
Silas yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pia atashiriki hafla ya kuingia makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na lvory Coast katika sekta ya michezo, inayotarajia kufanyika Aprili 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Soka Ndumbaro, waziri wa Ivory Coast wateta
Ndumbaro, waziri wa Ivory Coast wateta
Read also