Na mwandishi wetu
Timu ya Azam inatarajia kukwea pipa keshokutwa kuelekea Libya kwa ajili ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika ya mkondo wa kwanza dhidi ya Al Akhdar.
Azam ambayo inaanzia hatua ya pili ya michuano hiyo, itaanzia ugenini dhidi ya Akhdar ambao walifuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Al-Ahli Khartoum ya Sudan kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0.
Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria alisema kuwa wanashukuru kwa ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Singida United kwenye Ligi Kuu ya NBC ambao umewapa morali kuelekea kwenye michuano hiyo huku akisifia ushindani uliooneshwa na Singida umewaweka vizuri.
“Mpira ni kama vitu vingine, Singida wana wachezaji wazuri ambao wana ubora wa kucheza mashindano ya Afrika na wametupa changamoto kubwa, tunawapongeza Singida maana wametupa mechi nzuri yenye changamoto na sasa hiyo imeisha na inatupa fursa ya kuangalia mechi inayofuata.
“Sasa tutaondoka tarehe 6 kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika inayofuata, tutafika Libya siku hiyo hiyo na siku inayofuata tutapumzika kabla ya mechi yetu tarehe 8, tunatumaini kwamba tutumie mechi hii ili tupunguze mzigo kwenye mechi ya marudiano.
“Kwa sababu tunataka kwenda mbali kidogo tufike hatua ya makundi, tukipita hatua hii tutaangalia tutakutana na nani watakaokuja kutoka Ligi ya Mabingwa tutaona itakavyokuwa lakini tumejipanga kwa ajili ya hii michuano kisha tutaona mpira utakuwa na matokeo gani,” alisema Zakaria.
Baada ya mechi hiyo ya kwanza inayotarajiwa kupigwa Uwanja wa Martyrs, Benghazi, mchezo wa marudiano utapigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam mnamo Oktoba 16, mwaka huu.
Soka Azam yaelekea Libya kuivaa Al Akhdar
Azam yaelekea Libya kuivaa Al Akhdar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
