Na mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri huku akiwataka watendaji na wadau wa michezo kufanya tathmini zaidi ya namna ya kukuza na kuleta mafanikio zaidi kwenye michezo.
Mchengerwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa mashindano ya Afrika ya Gofu ya Wanawake (AACT) yaliyoshirikisha nchi 20 ambayo yalifanyika kuanzia Septemba 6 mpaka 8, mwaka huu kwenye viwanja vya Gymkhana.
Katika mashindano hayo Tanzania ilishika nafasi ya tatu, Morocco ilishika nafasi ya pili na nafasi ya kwanza ilikwenda Afrika Kusini.
“Naipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya tatu. Haya ni matunda ya uwekezaji mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye michezo katika kipindi kifupi cha uongozi wake, nahimiza na wengine waendelee kufanya vizuri ili tuendelee kuitangaza Tanzania,” alisema.
Pia aliipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Twiga Stars kwa kufanya vizuri na kufika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya COSAFA inayoendelea huko Afrika Kusini.
Mchengerwa alihimiza timu nyingine pia kufanya vizuri ili na kutoa wito kwa wadau wengine nchini kuendelea kudhamini ili kukuza vipaji vya michezo ili kusaidia kukuza na kuthamini vipaji mbalimbali nchini.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali na wadau wa michezo ikiwa ni pamoja na Balozi wa Morocco nchini, Zakaria El Goumiri na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu.
Soka Serikali kuzibeba timu zinazofanya vizuri
Serikali kuzibeba timu zinazofanya vizuri
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
