Na mwandishi wetu
Kiungo wa Yanga SC, Mganda Khalid Aucho amewataka wapenda soka wamfurahie kipindi hiki akiendelea kulisakata kabumbu katika Ligi Kuu ya NBC kwa sababu hakuna Aucho mwingine ambaye ataonekana kwenye soka la Bongo.
Aucho au ‘The Tank’ kama anavyofahamika na wapenzi wa soka nchini ameeleza hisia zake hizo kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram na pia kuonesha dhahiri namna gani anaikubali na kuipenda timu hiyo.
“Nifurahie wakati huu nikiwa kwenye ligi ya Tanzania, kwa sababu hautomuona Aucho Khalid mwingine tena. Muwe na wiki mpya yenye baraka,” ameandika kiungo huyo aliyewahi kuzitumikia timu za Baroka ya Afrika Kusini, Red Star ya Serbia na nyinginezo.
Aucho anayemudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji akiwa na uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati pia, huu ni msimu wake wa tatu tangu atue Yanga akitokea El Makasa ya Misri.
Katika kikosi cha kwanza cha Yanga ameendelea kuwa mchezaji muhimu na kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Soka Khalid Aucho yupo mmoja tu
Khalid Aucho yupo mmoja tu
Related posts
Read also