Na mwandishi wetu
Mabondia 16 wanatarajiwa kupanda ulingoni katika mapambano manane ya utangulizi kuelekea pambano la Selemani Kidunda dhidi ya Eric Mukadi wa DR Congo litakalopigwa Juni 30, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mbali ya Kidunda pia Mfaume Mfaume atapanda ulingoni kuzichapa na Mkululeko Mhlongo raia wa Afrika Kusini katika pambano la mwisho la utangulizi kabla ya Kidunda kupanda ulingoni kuhitimisha dhidi ya Mukadi.
Promota wa pambano hilo kutoka PAF Promotion Company Limited, Fadhili Maogola amesema kuwa maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri ambapo sasa mambo yamekamilika baada ya uwepo wa mapambano 10 usiku huo ikijumuisha mabondia 20 wakiwemo watatu kutoka nje ya Tanzania.
“Tunashukuru Mungu maandalizi ya pambano letu la Hata Usipolala Patakucha, yanaendelea vizuri na matarajio yetu ni kuona tunaenda kuijaza Mlimani City kwa kushuhudia pambano kubwa ndani ya mwaka huu ambalo litajumuisha mabondia wengi wakubwa kwa sasa likiwemo la Kidunda dhidi ya Mukadi,” alisema Maogola.
Mapambano hayo ya utangulizi yatawakutanisha Fadhili Majiha ‘Stopper’ dhidi ya Jamal Kunoga wakati Saleh Kasim atapambana na Said Bwanga kabla ya Deo Samweli kumvaa Adam Ngange.
Wengine ni Pius Mpenda atayeumana na Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama Jonh Cena akitarajia kupasuana na Yona Segu huku Omary Maulid atakung’utana na Shaban Kibiriti na Boniface Seguda ataminyana na Hamza Mahamoudu na Herry Rashid atamalizana na Hussein Pendeza.
Ngumi Kidunda, mabondia 16 ulingoni Juni 30
Kidunda, mabondia 16 ulingoni Juni 30
Read also