Na mwandishi wetu
Katika kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC, timu ya Namungo imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Hassan Kabunda aliyekuwa akikipiga KMC.
Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidady ameeleza kuwa wamekamilisha usajili huo kutokana na maelekezo ya benchi lao la ufundi linaloongozwa na Hanoor Janza na hivyo kumpa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili.
“Ni kweli tumekamilisha usajili wa Kabunda, ni mchezaji ambaye uwezo wake uliwavutia benchi letu la ufundi na uzuri ni kwamba tulipowafuata wenzetu wa KMC, hawakuleta tabu ukizingatia mchezaji mwenyewe alihitaji kubadilisha mazingira,” alisema Zidadu.
Zidadu alieleza kuwa baada ya kukamilisha usajili huo mchakato wa kukiimarisha kikosi chao bado unaendelea na hivi karibuni watayaweka hadharani majina ya wachezaji ambao wamemalizana nao ikiwemo wale wa kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa usajili wanaoufanya una lengo la kuirudisha Namungo kwenye ushindani wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na mikakati yao ni kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita ambapo walishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho na kutolewa katika hatua ya makundi.
Soka Kabunda amwaga wino Namungo
Kabunda amwaga wino Namungo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
