Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Morocco (pichani) amesema kwa sasa lango lake liko salama kwa asilimia 100 baada ya kutua kwa kipa Eric Johora katika kikosi hicho akitokea Yanga SC.
Morocco ameiambia GreenSports kuwa mbali na ubora aliokuwa nao kipa huyo aliyetambulishwa na timu hiyo lakini pia mafanikio na ujuzi alioupata akiwa Yanga ni jambo muhimu kwao.
“Ni kipa anayekuja kuongeza upinzani na kuliweka lango salama zaidi kutokana na ujuzi alionao, anatokea Yanga ambayo imekuwa ikishiriki michuano mingi na kufika mbali hivyo ujuzi wake pia ni jambo zuri zaidi kabla ya kugusa kipaji kikubwa alichonacho,” alisema Morocco.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars alieleza kutua kwa Johora sasa ni wazi wako hatua za mwisho kukamilisha usajili kuelekea msimu ujao, wakitarajia kuhitimisha kwa kuongeza beki mmoja pekee.
Wachezaji wengine waliosajiliwa na Geita mpaka sasa ni Carlos Protas, Tariq Seif, Samuel Onditi, Valentino Kusengama, Yusuf Dunia, Mwaite Gereza na Abeid Athuman.
Soka Morocco amfurahia kipa Geita
Morocco amfurahia kipa Geita
Read also
