Melbourne, Australia
Kocha mpya wa Man United, Erik ten Hag ameanza kunyoosha makucha yake katika kutafuta ubora wa kikosi chake na mtu wa kwanza kukumbana na makucha hayo ni nahodha wa timu hiyo, Harry Maguire ambaye amepewa angalizo akitakiwa awe makini vinginevyo anaweza kupoteza namba.
Ten Haag ametoa kauli hiyo wakati huu ambao Maguire amejikuta akizomewa na mashabiki wa timu hiyo ambao hawajaridhishwa na kiwango chake kwenye mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu wa 2022/23 dhidi ya Crystal Palace iliyopigwa leo mjini Melbourne, Australia na Man United kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
Maguire ameambiwa na Ten Haag kuwa kukubaliwa kuendelea na unahodha wa timu hiyo haina maana kwamba atakuwa na uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza badala yake ana kazi kubwa ya kupambana kudhihirisha uwezo wake.
Awali hata hivyo akimzungumzia mchezaji huyo, Ten Haag alisema, “Harry anavutia kiuchezaji na nategemea makubwa kwake, wakati wote naziona sifa za yeye kuwa nahodha.
“Kuijenga timu kwangu ni jambo muhimu, wakati wote huwa nazungumzia kuhusu kundi la viongozi, nahodha ni mtu muhimu sana na nafurahia Maguire kuwa nahodha,” aliongeza Ten Haag na kusisitiza kwamba mchezaji huyo anatakiwa kuipigania namba hasa kutokana na changamoto atakayoipata.
“Nafikiri ameshathibitisha uwezo wake siku za nyuma lakini anatakiwa kufanya hivyo na sasa na hata siku zijazo, nitampa msaada kila mahali kadri nitakavyoweza lakini mwisho wa siku ni yeye ndiye anayetakiwa kufanya vizuri na ana sifa zote za kufanya hivyo,” alisema Ten Haag.
“Lakini kuna ushindani wa ndani na hicho ndicho klabu ya hadhi ya Man United inachokihitaji, huwezi kushinda na wachezaji 11 pekee, tunahitaji kikosi hususan msimu huu tukiwa na mechi nyingi, tuna mabeki wazuri wa kati na Harry ni mmoja wao, anaweza kucheza kushoto, na kulia,” alisema Ten Haag.
Ujio wa Lisandro Martinez aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni 55.3 milioni akitokea Ajax utamuweka katika ushindani Maguire lakini pia atajikuta katika hali hiyo hiyo kutoka kwa Raphael Varane na Victor Lindelof katika nafasi ya beki wa kati.
Kimataifa Ten Haag ampasha Maguire
Ten Haag ampasha Maguire
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
