Barcelona, Hispania
Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez amesema itakuwa pigo kubwa kwa timu yake kutolewa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo.
Barcelona au Barca itakuwa imejiweka pagumu na katika mazingira ya kutolewa kwenye michuano hiyo mikubwa na yenye hadhi duniani kama itapoteza mechi yake ya leo Jumatano ya Kundi C dhidi ya Inter Milan kwenye dimba la Nou Camp na Bayern Munich kupata walau pointi moja katika mechi yake dhidi ya Viktoria Plzen.
Tofauti na hivyo ushindi utaifanya timu hiyo kuwa sawa pointi na Inter huku timu zote hizo zikiwa na kibarua kigumu katka mechi zijazo dhidi ya Bayern na baadaye dhidi ya Plzen, iwapo itatokea timu hizo kufungana pointi katika mechi zao sita, mechi baina ya timu hizo na mabao ya kufunga na kufungwa ndivyo vitu pekee vitakavyozitofautisha timu hizo katika kundi lao.
“Itakuwa pigo kubwa kutosonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa lakini kimsingi tunaangalia kwa mtazamo chanya,” alisema Xavi katika mkutano na waandishi wa habari.
“Kuna hali ya mkanganyiko kwa upande wetu lakini tutashambulia na kuwa makini tukipigania pointi tatu ili kuweka hai matumaini yetu katika mashindano haya, pointi tatu tu zitatutosha,” alisema Xavi.
Barca ina pointi tatu tu katika mech zake tatu za michuano hiyo msimu huu baada ya kushindwa kutamba mbele ya Bayern na Inter.
“Hali haiko vizuri kwetu, tulipoteza nafasi nyingi Munich na hapo hapo kukawa na utata wa mwamuzi kule Milan pamoja na kutofanya mashambulizi mengi lakini Jumatano inatupa nafasi ya kuweka sawa mambo yote,” alisema Xavi.
“Tuna vipaji na shauku ya kujibu mapigo kwa kile tulichokutana nacho Milan, natumaini hasira hizo zitakuwa msaada katika kucheza vizuri na kushambulia vizuri,” aliongeza Xavi ambaye licha ya mambo kutokuwa mazuri kwenye Ligi ya Mabingwa, timu yake inafanya vizuri kwenye La Liga.
Pamoja na matumaini anayojipa Xavi lakini timu yake leo huenda ikawakosa Jules Kounde, Ronald Araujo, Andreas Christensen, Hector Bellerin na Franck Kessie hapo hapo kukiwa na utata iwapo Memphis Depay atakuwa uwanjani au la.
Mechi za leo Jumatano za Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Napoli v Ajax
Rangers v Liverpool
Atlético Madrid v Club Bruges
B. Leverkusen v FC Porto
Barcelona v Inter Milan
Viktoria Plzen v Bayern Munich
Sporting Lisbon v Marseille
Tottenham v Eintracht Frankfurt
Kimataifa Xavi: Kutolewa Ligi ya Mabingwa pigo kubwa
Xavi: Kutolewa Ligi ya Mabingwa pigo kubwa
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
