Na mwandishi wetu
Hatma ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kama ataruhusiwa kuvunja mkataba na Yanga itajulikana Jumatatu, siku ambayo pia mchezaji huyo ataamua kama analifikisha suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) au ataridhia kitakachoamuliwa.
Jumamosi hii Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliamua mchezaji huyo kwa sasa anabaki kuwa wa Yanga lakini ikaahidi kuwa uamuzi kamili kuhusu pande zote mbili utatangazwa Jumatatu hii yaani, Juni 9.
Uamuzi huo unaacha maswali ya nini kitakachoamuliwa Jumatatu kuhusu sakata hilo lakini kwa vyovyote vile itakavyokuwa nafasi ya Fei kuelekea au kutoelekea CAS kimsingi itatokana na kitakachoamuliwa Jumatatu.
Maswali mengi ambayo yanatatiza wadau wa soka nchini ni kuhusu uamuzi huo wa TFF kwa nini umekuwa nusu haukumaliza kila kitu, nini hasa ambacho imeshindikana kutangazwa Jumamosi hadi kuwe na ulazima wa kukitangaza Jumatatu.
Mashabiki wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu kupata ufafanuzi wa kina wa sakata la mchezaji huyo ambalo limeendelea kuwa mjadala lakini wakaishia kukutana na taarifa ya TFF yenye aya nne ambayo imewaachia maswali.
Jumatatu si mbali, hapo ndipo wadau watakapojua kama Fei ambaye inaonekana amedhamiria kuondoka Yanga atafanikisha hilo au atalazimika kuisaka dhamira hiyo CAS.
Soka Hadithi ya Fei Toto, CAS Jtatu
Hadithi ya Fei Toto, CAS Jtatu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
