Nice, Ufaransa
Kocha wa PSG, Christophe Galtier (pichani) na mtoto wake wamekamatwa wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu tuhuma za ubaguzi wa rangi katika klabu ya zamani aliyokuwa akiinoa kocha huyo.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka mmoja nchini Ufaransa, Galtier na mtoto wake, John Valovic-Galtier walikamatwa Ijumaa asubuhi na kuhojiwa kwa saa kadhaa.
Galtier ambaye zipo habari kwamba huenda PSG ikaachana naye ingawa kwa sasa bado ana mkataba na timu hiyo, alikanusha tuhuma za kutoa kauli za ubaguzi dhidi ya Waislam wakati akiwa kocha wa klabu ya Nice wakati tuhuma hizo zilipoibuliwa Januari mwaka huu
Habari zaidi zinadai kwamba katika moja ya mawasiliano aliyofanya na vigogo wa klabu ya Nice, Galtier anatuhumiwa kusema kwamba katika kikosi chake kuna wachezaji wengi weusi wenye asili ya Afrika pamoja na waislam.
Katika taarifa iliyotolewa baadaye na Galtier kupitia mwanasheria wake, kocha huyo alieleza jinsi alivyoshtuka baada ya kubaini kuwapo tuhuma za udhalilishaji na kuahidi kuchukua hatua za kisheia ambazo hata hivyo hakuziweka wazi.
Kimataifa Kocha PSG akamatwa kwa ubaguzi
Kocha PSG akamatwa kwa ubaguzi
Read also