Valencia, Hispania
Kiungo mkabaji mbabe wa zamani wa AC Milan na timu ya Taifa ya Italia, Gennaro Gattuso amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa klabu ya Valencia ya Hispania.
Gattuso mwenye umri wa miaka 44, amekuwa bila timu tangu Mei mwaka jana alipoachana na klabu ya Napoli aliyokuwa akiinoa ambayo aliiwezesha kutwaa taji la Copa Italia.
Majira ya kiangazi mwaka jana, Gattuso alitangazwa kuwa kocha wa timu ya Fiorentina lakini katika hali ya kushangaza aliachana na timu hiyo kabla hata siku yake ya kuanza kazi rasmi kufika.
Katika historia yake ya soka la ushindani kabla ya kuugeukia ukocha, Gattuso alitamba na AC Milan kwa takriban miaka 13 akijipatia sifa ya kuwa kiungo mahiri na mbabe na sasa anachukua majukumu ya kuinoa Valencia baada ya kutimuliwa kwa kocha Jose Bordalas Ijumaa iliyopita.
Valencia ambayo imewahi kutwaa taji la La Liga mara sita, ilimaliza msimu huu wa ligi hiyo ikiwa nafasi ya tisa na hivyo Gattuso ana kazi kubwa ya kuibadili timu hiyo na kuiweka kwenye ushindani kuanzia Hispania hadi Ulaya.
Kimataifa Mbabe Gattuso kocha mpya Valencia
Mbabe Gattuso kocha mpya Valencia
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
