Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema siku zilizobaki zinamtosha kuwapa wachezaji wake mbinu zitakazowapa ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Kikosi cha Yanga kimeingia kambini jana Avic Town, Kigamboni kujiandaa kuikabili miamba hiyo ya Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya kwanza utakaochezwa Machi 30 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
“Hakuna kinachoshindikana, wapinzani miaka ya karibuni wamekuwa kwenye kiwango bora lakini hata Yanga siyo timu ndogo ndio maana tupo kambini kuhakikisha tunajiandaa na kupanga mikakati madhubuti itakayotupa furaha baada ya dakika 180,” alisema Gamondi.
Alisema hawatishwi na mafanikio ya Mamelodi sababu hadi kufika hapo wamekutana na timu kubwa zenye ‘levo’ yao na wamepambana nazo na nyingine kuzifunga kwa hiyo wanachokifanya hivi sasa ni kuweka mitego ili wapinzani wao wanase na kuwapa furaha mashabiki wao na Watanzania.
Kocha huyo raia wa Argentina alisema anaridhishwa na maendeleo ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi akiwemo kiungo Khalid Aucho na Pacome Zouzoua na anaamini hadi siku ya mchezo watakuwa tayari kwa ajili ya kutumika.
Gamondi alisema anaamini Yanga inakwenda kutengeneza rekodi nyingine kubwa Afrika kwa kuitoa Mamelodi na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabigwa Afrika msimu huu.
Kimataifa ‘Muda wa kuikabili Mamelodi unatosha’
‘Muda wa kuikabili Mamelodi unatosha’
Read also