Madrid, Hispania
Tuhuma za klabu ya Barcelona kutoa rushwa kwa waamuzi zimechukua sura mpya baada ya polisi nchini Hispania kuvamia ofisi ya kamati ya waamuzi kama sehemu ya uchunguzi wa kashfa hiyo.
Barcelona au Barca inakabiliwa na kashfa ya kutoa malipo yanayotiliwa shaka kwa makamu mwenyekiti wa zamani wa kamati ya waamuzi, Jose Maria Negreira ili kuibeba timu hiyo katika mechi zake.
Barca hata hivyo imekana kufanya kosa lolote na ingawa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa baada ya polisi kuvamia ofisi hizo zilizopo mjini Madrid, Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) nao unaifanyia uchunguzi kadhia hiyo.
Awali tuhuma dhidi ya Barca ziliwalishwa na ofisi ya waendesha mashtaka ya Barcelona mwezi Machi mwaka huu na siku kadhaa baadaye, Uefa nao wakatangaza kuanza uchunguzi wao.
Katika madai hayo, Barca wanatuhumiwa kumlipa Negreira Pauni 7.4 milioni kati ya mwaka 2016 na 2018 kupitia kampuni yake ya Dasnil 95, malipo ambayo uchunguzi wa awali uliyahusisha na ukwepaji wa kodi wa kampuni hiyo inayoongozwa na Negreira.
Barca hata hivyo ilikiri kutoa malipo hayo kwenye kampuni ya Dasnil 95 lakini ilidai kwamba malipo hayo yalikuwa ni kwa ajili ya kuandika ripoti maalum ya waamuzi kwa njia ya video, ripoti ambayo iliombwa na benchi la ufundi la klabu hiyo.
Katika ufafanuzi wake klabu hiyo ilidai kwamba malipo kwa ajili ya ripoti za aina hiyo ni jambo la kawaida kufanywa na klabu profesheno.
Kimataifa Kashfa ya Barca kuhonga waamuzi yachukua sura mpya
Kashfa ya Barca kuhonga waamuzi yachukua sura mpya
Read also