Bremen, Ujerumani
Mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane ameweka rekodi mpya ya mabao kwa kufikisha mabao 500 katika soka la ushindi, mabao 100 kati ya hayo akiyafunga kwa penalti.
Kane amefikisha rekodi hiyo ya mabao baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 ambao Bayern imeupata Jumamosi Februari 14, 2026 katika mechi ya Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga dhidi ya Werder Bremen.
Katika mechi na Bremen, Kane alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 22 baada ya Senne Lynen kumchezea rafu Lennart Karl wa Bayern katika eneo la penalti.
Kane, 32, ambaye hilo ni bao lake la tisa analofunga kwa penalti msimu huu, aliongeza bao la pili dakika nne baadaye, bao lililomfanya afikishe mabao 500 katika mechi 743 za klabu na timu ya taifa.
Bao la tatu na la ushindi kwa Bayern lilifungwa na Leon Goretzka katika dakika ya 70 na kuihakikishia timu hiyo ushindi ambao umeifanya kushika usukani katika Bundesliga kwa tofauti ya pointi sita.
Kwa msimu huu pekee, Kane hadi sasa ameifungia Bayern mabao 41, kati ya hayo 26 ni ya kwenye ligi na mengine katika mashindano mengine ya Ujerumani na Ulaya.
Kimataifa Kane afikisha mabao 500
Kane afikisha mabao 500
Read also
