Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ametajwa tena kwenye jarida la Forbes kuwa anashika namba 13 Afrika kwa utajiri akifungana na matajiri wengine wawili katika nafasi hiyo.
Katika orodha hiyo mpya ya mwaka huu, Dewji ameelezwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni) kama ilivyo kwa Youssef Mansour raia wa Misri na Othman Benjelloun wa Morocco.
Dewji ambaye ametajwa kama bilionea mwenye umri mdogo zaidi kwa miaka sita mfululizo iliyopita pia kwenye orodha ya mwaka jana alitajwa kushika namba 15 akiwa na kiwango hicho hicho cha fedha.
Katika orodha hiyo yenye watu 19 ikiwa ni ongezeko la mtu mmoja tofauti na mwaka jana, Rais wa Shirikisho la Soka (Caf), Patrice Motsepe naye ametajwa akiwa namba tisa na utajiri wa Dola 3.2 bilioni.
Aliko Dangote raia wa Nigeria ameendelea kushikilia nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola 13.5 bilioni, nafasi ya pili ni ya Johann Rupert na familia yake kwa utajiri wa Dola 10.7 bilioni huku Nicky Oppenheimer na familia yake wakikamilisha tatu bora kwa utajiri wa Dola 8.4 bilioni.
Soka Forbes wamtaja tena Mo Dewji
Forbes wamtaja tena Mo Dewji
Read also
