Paris, Ufaransa
Thiago Silva amesema kwamba anaamini nyota mwenzake wa Brazil, Neymar anatakiwa kuondoka katika klabu ya PSG ya Ufaransa na kuhamia England na kuungana naye katika klabu ya Chelsea..
Mambo ya baadaye na Neymar ndani ya PSG yameendelea kuwa mjadala katika wiki za karibuni huku kukiwa na habari kwamba klabu hiyo iko tayari kumuuza mchezaji huyo katika kipindi hiki cha usajili huku Chelsea wakitajwa kumpigia hesabu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 sasa.
“Neymar anatakiwa kwenda Chelsea, kama hilo litafanikiwa litakuwa jambo zuri, naamini litafanikiwa lakini sifahamu lolote kuhusu mpango huo,” alisema Silva ambaye aliwahi kucheza na Neymar wakiwa , PSG chini ya kocha wa sasa wa Chelsea, Thomas Tuchel.
Neymar ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017 kwa ada ya Euro milioni 222 akitokea Barcelona, hadi sasa ameichezea timu hiyo kwa misimu mitano, mbali na Chelesea, mara kadhaa amekuwa akihusishwa na mipango ya kurudi klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Neymar pamoja na ubora wake lakini amekuwa katika kipindi kigumu PSG na hivi karibuni yeye na wachezaji wenzake mastaa walijikuta wakizomewa na mashabiki baada ya timu hiyo kutolewa na Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.
Kimataifa Silva amtaka Neymar Chelsea
Silva amtaka Neymar Chelsea
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
