Na Joseph Shaluwa
Msanii maarufu nchini Nigeria, Cobhams Asuquo (pichani) ameshirikiana na kundi maarufu nchini Kenya la Sauti Sol kwenye video inayokwenda kwa jina la ‘Lady Fiona’.
Cobhams ambaye pia ni mwandishi wa mashairi na mtayarishaji muziki, ameunganisha nguvu na miamba ya muziki nchini Kenya, Sauti Sol ambao wameshikilia tuzo ya kundi bora la muziki wa Afro-Pop, Kenya.
Huu ni ushirikiano mzuri wa kimataifa unaowakutanisha miamba ya muziki barani Afrika na kuunganisha pamoja sauti zao tamu zinazotoa burudani ya aina yake kwa hadhira.
“Lady Fiona” ni wimbo wa aina yake wenye mahadhi ya Afro-pop, unaotoa nafasi ya ubunifu wa wasanii hawa – Cobhams Asuquo na Sauti Sol,” inaeleza sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari.
Ni wimbo unaowafanya wasikilizaji wazame katika ulimwengu wa mahaba na kuibua hisia zinazoweza kumpata mtu yeyote ambaye amepitia furaha au magumu katika mahusiano ya kimapenzi.
“Ombi letu kubwa kwa mashabiki wa muziki ni kuitazama video hiyo ambayo tayari inapatikana mitandaoni. Hapo ukweli wa haya tunayosema utathibitika,” ilihitimisha taarifa hiyo.
Burudani Cobhams agonga kolabo na Sauti Sol
Cobhams agonga kolabo na Sauti Sol
Related posts
Read also
