Na mwandishi wetu
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatimaye imepata ushindi katika michuano ya Fifa Series 2024 inayofanyika nchini Azerbaijan baada ya kuichapa Mongolia mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa leo Jumatatu.
Stars ambayo imetoka kuchapwa na Bulgaria bao 1-0 karika michezo hiyo, leo iliandika bao lake la kwanza dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Kelvin John.
Kelvin akiwa na jezi namba 10 mgongoni, jezi ambayo imezoeleka kuvaliwa na nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta, alifunga bao hilo akiitumia vizuri pasi Ben Starkie.
Abdul Sopu aliiandikia Stars bao la pili katika dakika ya 62 akiitumia vizuri pasi ya mchezaji mwenzake wa Azam FC, Feisal Salum au Fei Toto.
Baada ya kuingia mabao hayo, kocha wa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Himid Mao na Fei Toto na nafasi zao kuingia Yahya Zayd na Morrice Abraham.
Mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Stars ambayo iliandika bao la tatu katika dakika ya 76, bao ambalo lilifungwa na Novatus Dismas akiitumia pasi ya Sopu.
Kimataifa Stars yainyuka Mongolia 3-0
Stars yainyuka Mongolia 3-0
Read also