Na mwandishi wetu
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watuhumiwa 11 akiwemo kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultani ‘Shilton’ (40).
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya (pichani juu) alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa za kulevya aina ya bangi kama moja ya malighafi.
Watuhumiwa wengine ni Kambi Zubeir Seif ambaye ni mfanyabishara na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso kilichopo Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam, John John ‘Chipanda’ ambaye jukumu lake ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sports Academy.
Pia wamo Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu ‘Mbonde’ mkazi wa Kisemvule, Rajabu Dhahabu mkazi wa Tabata, Seleman Matola Said mkazi wa Temeke Wailes, Hussein Pazi na Ramadhani Chalamila mkazi wa Kongowe.
Kwa mujibu wa DCEA, ukamataji wa watuhumiwa hao ulifanikishwa kutokana na operesheni waliyoiendesha hivi karibuni kwenye maeneo mbalimbali nchini kati ya mwezi Oktoba na Novemba.
Soka Msako DCEA wamnasa kocha Simba
Msako DCEA wamnasa kocha Simba
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
