Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema msimu uliomalizika hivi karibuni wa 2022-23 haukuwa mzuri kwake kutokana na changamoto alizopitia lakini anaamini msimu ujao atakuwa vizuri zaidi.
Ajibu amesema hayo akifafanua kuwa timu yake ya Singida imekuwa na wakati mzuri na kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne lakini kwake majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili yamemkwamisha.
“Msimu kwa ujumla ulikuwa mzuri ukizungumzia kitimu, timu imefanya vizuri na kumaliza nafasi za juu lakini kwa upande wangu binafsi haukuwa mzuri, sikuwa na furaha maana nimekaa nje miezi miwili sasa kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiniandama, ingawa sasa nimeanza kukaa vizuri,” alisema Ajibu.
Kiungo huyo alisema tayari ameanza kujifua kwenye viwanja tofauti tofauti kutafuta utimamu wa mwili kabla ya kujiunga na timu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu NBC pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Pia, Ajibu aliyewahi kutamba na timu za Simba na Yanga kabla ya kutimkia Azam anaamini msimu ujao atafanya vizuri kwa namna anavyojipanga kwa ajili ya kuisaidia Singida kufikia malengo iliyonayo.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye ligi kwa msimu wa pili mfululizo tangu ilipopanda msimu uliopita na pia kufika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Soka Ajibu akiri mambo magumu
Ajibu akiri mambo magumu
Read also