Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kutembeza vichapo katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Singida Fountain Gate mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Jumapili hii jioni kwenye dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 55 katika mechi 21 na kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo ikiiacha Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nane.
Mpinzani mwingine wa Yanga katika mbio za kulisaka taji la ligi hiyo, Simba imeendelea kuwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 wakati Singida iliyotokwa kufungwa na Yanga inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 24.
Yanga walianza kuliona lango la Singida katika dakika ya 41 baada ya Joseph Guede kufumua shuti lililojaa wavuni na kuifanya timu hiyo iende mapumziko ikiwa kifua mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili, Singida walikianza kwa kasi na kuonesha dalili zote za kusaka bao la kusawazisha lakini kasi hiyo iliyowachukua dakika 10 hadi 15 haikuweza kulitetemesha lango la Yanga.
Yanga waliandika bao la pli katika dakika ya 65 mfungaji akiwa ni Stephanie Aziz Ki kwa shuti kali akiitumia vizuri pasi ya Clement Mzize kufunga bao hilo.
Dakika tatu baadaye, Guede alizidi kuwakatisha tamaa Singida baada ya kufunga bao la pili kwa kichwa akineemeka na pasi ya Mzize.
Akizungumzia matokeo hayo, kocha wa Singida, Ngawina Ngawina alisema kwamba wachezaji wake walifanya makosa ambayo Yanga waliyatumia kuwaadhibu.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa mjini Lindi, Azam iliyokuwa ugenini ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo FC.
Soka Yanga yaichakaza Singida 3-0
Yanga yaichakaza Singida 3-0
Read also