Montevideo, Uruguay
Kinara wa mabao wa timu ya Taifa ya Uruguay ambaye pia amewahi kutamba na klabu za Barcelona na Liverpool, Luis Suarez sasa ameamua kurudi katika klabu yake ya zamani ya Nacional ya Uruguay.
Suarez ambaye ameifungia timu ya Taifa ya Uruguay jumla ya mabao 68 katika mechi 132 amejiunga na Nacional akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka katika klabu ya Atletico Madrid mkataba wake ukiwa unafikia ukomo katika kipindi hiki.
Nacional ambayo imemaliza Ligi Kuu Uruguay maarufu Primera Division ikiwa nafasi ya pili hata hivyo haikutaja undani wa mkataba huo na marupurupu atakayoyapata mchezaji huyo. “Najivunia kuvaa kwa mara nyingine jezi yangu ya Nacional, asanteni kwa kuniunga mkono, tutaonana,” alisema Suarez kupitia mitandao ya kijamii.
Mashabiki wa Nacional zaidi ya 20,000 walivaa vazi maalum la mchezaji huyo katika mechi ya hivi karibuni ya timu hiyo uvumi wa mchezaji huyo kurudi Nacional ukiwa umepamba moto wakati kwa klabu ya Nacional kwenye taarifa yake kupitia mitandao ya kijamii ilisema, “Tuna furaha kuwa na wewe nyumbani.
Suarez alianza kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Nacional mwaka 2005 akiwa na miaka 18 na kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la Primera Division akiwa amefunga mabao 10 katika mehi 27 za ligi na baada ya hapo alijiunga na klabu ya Groningen ya Uholanzi kiha akaelekea Ajax mwaka uliofuata na baada ya hapo alijiunga na Liverpool mwaka 2011 kabla ya kujiunga na Barcelona mwaka 2014.
Akiwa na Barcelona hadi alipoondoka mwaka 2020 amebeba mataji ya La Liga mara nne na kujiunga na Atletico ambapo pia amefanikiwa kubeba taji la La Liga katika msimu wake wa kwanza akiwa amefunga mabao 21 katika mechi 32.
Kimataifa Suarez arudi nyumbani Nacional
Suarez arudi nyumbani Nacional
Related posts
Read also