Milan, Italia
Winga wa zamani wa Man United, Angel di Maria amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Juventus ya Italia akitokea PSG ya Ufaransa.
Di Maria, 34, ambaye ameondoka PSG akiwa mchezaji huru, mwaka 2014 alijiunga na Man United akitokea Real Madrid kwa ada iliyoweka rekodi ya uhamisho ya Pauni 59.7 lakini mwaka 2015, Man United nao walimuuza PSG kwa ada ya Pauni 44.3 milioni.
Akiwa PSG ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu Ufaransa au Ligi 1 akiwa amefunga mabao 92 katika mechi 295 lakini msimu uliopita mambo yake kidogo hayakuwa mazuri kwani alicheza mechi 26 na kufunga mabao matano tu.
Hatua ya Di Maria kuondoka PSG inaamika kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na matajiri wa timu hiyo ambao hawajaridhika na mafanikio ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata licha ya uwekezaji mkubwa ambao wameufanya na hivyo hawakuona sababu ya kumuongezea mkataba.
Nyota mwingine wa timu hiyo ambaye naye huenda akahama ni Neymar ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na timu nyingine za England na Hispania ikiwamo timu yake ya zamani ya Barcelona.
Katika msimu ulioisha hivi karibuni wa 2021/22, PSG ilitolewa kwenye fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora hali iliyowakera matajiri wa timu hiyo pamoja na mashabiki ambao walifikia hatua ya kuwazomea wachezaji wao.
Kimataifa Di Maria asaini Juventus
Di Maria asaini Juventus
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
