Porto, Ureno
Baada ya kushutumiwa kwa kutoka uwanjani kabla ya mechi ya Man United na Tottenham Hotspur kumalizika, winga Cristiano Ronaldo amemgeuzia kibao kocha wake, Erik ten Hag akisema kuwa ndiye chanzo cha tatizo hilo.
Ronaldo alisema alijiona amekosewa heshima na kocha huyo baada ya kumwambia hatolazimika kumpa nafasi kuingia kipindi cha pili katika mechi na Man City na baadaye akajaribu kumtuliza kwa kumpa nafasi dakika tatu kabla ya kumalizika mechi na Spurs jambo lililomfanya mchezaji huyo kususa na kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mechi hiyo kumalizika.
“Hunipi nafasi ya kucheza dhidi ya Man City kwa sababu huheshimu soka langu, na baadaye unataka kunipa dakika tatu nicheze mechi dhidi ya Tottenham, hii haiingii akilini, nafikiri alifanya hivyo makusudi, naona alinikasirisha, si kwenye mechi hiyo tu bali kabla ya hapo,” alisema katika sehemu ya mahojiano aliyofanya hivi karibuni.
“Hanipi heshima ambayo natakiwa kupewa, lakini hali hivyo ndivyo ilivyo, na ndio maana katika mechi na Tottenham niliondoka, kocha haniheshimu, na ndio maana uhusiano wetu upo hivyo ulivyo, mara kwa mara anazungumza kwenye vyombo vya habari anakuja kwangu na ananikubali na maneno mengine mengi yasiyo na maana, lakini hiyo ni kwenye vyombo vya habari kwa asilimia 100.”
Ronaldo ambaye leo Ijumaa anatarajia kuwasili Qatar akiwa na kikosi cha timu ya Ureno kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia, kwa ambacho amekuwa akikisema ni vigumu kusema kama anaweza kuendelea kuwa mchezaji wa Man United baada ya fainali za Kombe la Dunia.
Pamoja na kutojua hatma yake Man United, nyota huyo wa zamani wa klabu za Real Madrid na Juventus alikanusha habari kwamba hakuna klabu zinazotaka kumsajili na kwamba ofa pekee aliyopata ni kutoka Saudi Arabia.
“Kile ambacho wamekuwa wakisema miezi mitatu iliyopita ni uwongo na uchafu, wanasema wamenipa ofa hii na ile na wakurugenzi na marais (wa klabu) wamezungumzia kukataa kunisajili, ni uwongo mkubwa, kwani hicho sicho kilichotokea, kuna klabu, ni chache zinazotaka kunisajili na sikwenda kwa sababu nilijiona hapa ndio sahihi, huo ndio ukweli,” alisema Ronaldo.
“Kinachosemwa kwamba sitakiwi ni uchafu, ukweli ni kwamba nilifurahia kuwa hapa, nilishawishika kuwa na msimu mzuri hapa lakini wamekuwa wakirudia kusema kwamba hakuna anayemtaka Cristiano, ni vipi wasimtake mchezaji aliyefunga mabao 32 mwaka jana?” Alihoji Ronaldo.
Akizungumzia kuhusu uwezekano wa kustaafu timu ya Taifa, Ronaldo alisema kwamba atafanya hivyo hapo hapo iwapo Ureno itashinda Kombe la Dunia lakini kama hilo halitotokea mpango wake ni kucheza kwa miaka mingine mitatu hadi atakapofika miaka 40.
Kimataifa Ronaldo amshushia tuhuma mpya Ten Hag
Ronaldo amshushia tuhuma mpya Ten Hag
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
