Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Fred Minziro (pichani) amesema watautumia ushindi walioupata dhidi ya Mtibwa Sugar kama chachu ya kufanya vizuri katika mechi zao zijazo.
Wiki iliyopita maafande hao walipata ushindi wao wa kwanza msimu huu ambao uliwatoa mkiani na kupanda hadi nafasi ya 13 wakifikisha pointi nne kwa kuifunga Mtibwa mabao 3-2.
Minziro alikiri kuwa kupoteza mechi tatu mfululizo kuliwaweka katika wakati mgumu yeye na wachezaji wake lakini ushindi dhidi ya Mtibwa umewaongezea ari ya kupambana na kufanya vizuri mechi zinazofuata.
“Tulikuwa na mwanzo mbaya uliotokana na ushindani uliopo msimu huu lakini hatujakata tamaa, tumeendelea kurekebisha makosa yetu katika kila mchezo na juzi tumepata ushindi wetu wa kwanza ambao naamini utapandisha ari za wachezaji wangu ili tufanye vizuri mechi zijazo,” alisema Minziro.
Minziro alisema lengo lake kubwa akiwa na timu hiyo msimu huu ni kuhakikisha wanamaliza msimu kwenye nafasi za juu na siyo kujinusuru kushuka daraja kama ilivyokuwa misimu ya hivi karibuni.
Soka Mtibwa yaitia mzuka Prisons
Mtibwa yaitia mzuka Prisons
Read also