London, England
Klabu ya soka ya Arsenal hatimaye imekamilisha usajili wa mshambuliaji Mbrazil, Gabriel Jesus ambaye amejiunga na timu hiyo rasmi akitokea Manchester City kwa ada ya Pauni 45 milioni.
Jesus anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na kocha Mikel Arteta wa Arsenal katika wiki za hivi karibuni akiwa tayari amewasajili, kiungo Fabio Vieira, kipa Matt Turner na Mbrazil mwingine, Marquinhos ambaye ni mshambuliaji.
Arteta alielezea namna alivyofurahishwa na usajili huo akisema klabu imefanya jambo zuri kukamilisha usajili wa mchezaji wa hadhi ya Jesus katika klabu hiyo hasa kwa kuwa anaufahamu vizuri uwezo wake kwani aliwahi kuwa kocha wa mchezaji huyo wakati Arteta akiwa kocha msaidizi Man City.
Moja ya mambo ambayo Arteta amekuwa akiyafanya katika klabu hiyo kwenye usajili ni kuimarisha safu ya ushambuliaji hasa baada ya kuondoka kwa washambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette ambao waliondoka wakiwa wachezaji huru.
“Mimi binafsi namjua vizuri Gabriel na sote tunamjua vizuri kwa kipindi ambacho amekuwa kwenye Ligi Kuu England na hakika amekuwa na mafanikio hapa,” alisema Arteta.
“Huyu ni mchezaji ambaye tumekuwa tukimuwinda kwa kipindi kirefu na tumefanikiwa kupata mchezaji ambaye sote tulikuwa tukimtafuta, kwa hiyo nina furaha,” aliongeza Arteta akimzungumzia Jesus ambaye amekuwa Man City kwa kipindi cha miaka mitano na nusu.
Jesus ambaye akiwa Arsenal, atavaa jezi namba tisa, ameichezea Man City mechi 236 na kufunga mabao 95 huku akibeba mataji matatu ya Ligi Kuu England, matatu ya ligi na moja na FA.
Kimataifa Jesus rasmi mali ya Arsenal
Jesus rasmi mali ya Arsenal
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
