Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid inajipanga kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland wakati wa majira ya kiangazi baadaye mwaka huu.
Haaland mwenye umri wa miaka 22 anakuwa sehemu ya mpango mpya wa Real Madrid kusajili wachezaji nyota vijana wa bei mbaya watakaolinda hadhi ya timu hiyo barani Ulaya.
Katika mpango huo, Real Madrid pia inadaiwa kuwa katika hatua za awali ikiwania kumsajili kiungo wa England na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Jude Bellingham.
Hii si mara ya kwanza kwa Real Madrid kuhusishwa na mipango ya kumsajili Haaland ambaye ametokea kuwa tishio katika Ligi Kuu England akiwa ndiye kinara wa mabao wa ligi hiyo pamoja na klabu yake.
Tofauti na habari za siku za nyuma, safari hii muda maalum wa kumsajili Haaland umetajwa ikimaanisha kwamba msimu ujao atavaa jezi nyeupe ya Real Madrid na kuachana na jezi ya bluu ya Man City.
Inadaiwa katika usajili wa Haaland kuna kipengele kinachompa nafasi ya kujiunga na Real Madrid hapo baadaye ingawa kocha wa Man City, Pep Guardiola amewahi kukanusha kuwapo kipengele hicho.
Kuhusu Bellingham, habari zinadai kuwa Dortmund haitosita kumruhusu mchezaji huyo ahamie Real Madrid iwapo maslahi ya pande zote yataangaliwa kwa mapana yake.
Kimataifa Haaland kutua Madrid majira ya kiangazi
Haaland kutua Madrid majira ya kiangazi
Read also
