London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte anatarajia kufanyiwa upasuaji wa kibofu. Klabu yake imethibitisha hilo hii leo Jumatano.
Conte ambaye alijiunga na timu hiyo mwaka 2021 alikutwa na uvimbeuchungu karibu na kibofu na kujisikia vibaya zaidi ikiwa ni maumivu ya tumbo
“Kila mmoja katika klabu anamtakia heri kocha apone haraka,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo na kufafanua kwamba kocha huyo atarudi baada ya kumaliza matibabu.
Mechi ijayo ya Spurs itakuwa Jumapili ijayo nyumbani dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu England, mechi ambayo ni muhimu kwa timu hiyo kushinda ili kuimarisha nia yake ya kubaki katika nne bora au top four.
Spurs kwa sasa inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 36, imezidiwa na vinara na mahasimu wao wa jiji la London, Arsenal kwa tofauti ya pointi 14.
Hivi karibuni Conte alinukuliwa akijivua lawama baada ya kuulizwa kuhusu matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo ambapo alisema asilaumiwe peke yake bali waulizwe watu wengine kwenye timu wakiwamo madaktari na maofisa wengine.
Kimataifa Conte kufanyiwa upasuaji
Conte kufanyiwa upasuaji
Read also