Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa mshambuliaji wa Kagera Sugar, Anwar Jabir ‘Falcao’ ameongezewa muda zaidi wa majaribio kwenye klabu ya KAA Gent inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji.
Awali mshambuliaji huyo aliyetua Ubelgiji tangu Aprili 4, mwaka huu alipewa programu ya majaribio na timu hiyo kwa wiki mbili lakini sasa ameongezewa muda kwa ajili ya kuangaliwa zaidi.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime leo Jumamosi amesema kuwa maendeleo ya Falcao ni mazuri na kuna programu mpya amepewa ambayo ataifanya kwa siku chache ingawa hakueleza ni kwa kipindi cha muda gani.
“Anwar ameongezewa muda kule Ubelgiji, ni kweli wiki mbili zimekwisha lakini kuna programu nyingine ambayo wao wenyewe wametaka aifanye kwa muda kabla ya kumaliza rasmi majaribio yake,” alisema.
“Kwa kifupi anaendelea kufanya vizuri na sisi tumekuwa tukimwombea aendelee kufanya hivyo na tunaamini programu aliyopewa sasa ndiyo itakuwa programu yake ya mwisho ambayo itafanyika kwa siku chache tu,” alisema Maxime.
Endapo Falcao atafaulu majaribio yake hayo atakuwa mchezaji wa nne Mtanzania kukipiga Ubelgiji baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na Kelvin John wanaokipiga KRC Genk na Novatus Dismas wa Zulte Waregem.
Soka Anwar Jabir aongezewa muda Gent
Anwar Jabir aongezewa muda Gent
Read also
