Liverpool, England
Baada ya mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe kukataa kujiunga na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia, Liverpool imetia mguu ikidaiwa kukaa mezani na mchezaji huyo kwa lengo la kumsajili kwa mkopo.
Al Hilal hivi karibuni ilitangaza kumtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa ada ya Pauni 259 milioni ambayo ni rekodi ya dunia lakini Mbappe hakuwa tayari kwa jambo hilo.
Uamuzi huo wa Mbappe umewaamsha Liverpool ambao waliwahi kuhusishwa na mshambuliaji huyo lakini hawakulipa umuhimu jambo hilo na sasa wanaamini ni wakati sahihi wa kulifanyia kazi kwa nguvu zote.
Liverpool hata hivyo watakuwa na kazi ngumu kwani baada ya dili la Al Hilal kukwama, Real Madrid nao wanaamini huu ni wakati wao wa kumpata mshambuliaji huyo waliyemkosa msimu uliopita.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini Hispania, Real Madrid inadaiwa wametengeza kitita cha Pauni 198 milioni ili kumpata mshambuliaji huyo ambaye kwa hali ilivyo ni lazima aondoke PSG.
Mbappe ameingia katika mgogoro na mabosi wa PSG baada ya kumtaka achague moja kama ni kusaini mkataba mpya wakati huu na kama hataki aondoke.
Msimamo huo ni tofauti na ule wa Mbappe ambaye alisema hayuko tayari kusani mkataba mpya kwa sasa lakini anapenda kuendelea kuichezea timu hiyo. Mkataba wa Mbappe na PSG unafikia ukomo mwakani.
PSG haipo tayari kumuona Mbappe anaendelea kuwa na timu hiyo bila mkataba mpya kwani hiyo maana yake ni kwamba mwakani ataondoka akiwa mchezaji huru na wao hawatolipwa chochote.
Kimataifa Liverpool yamuita Mbappe mezani
Liverpool yamuita Mbappe mezani
Read also