Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephen Aziz Ki amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumpigia kura zilizomwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba.
Mchezaji huyo ameshinda tuzo hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kujinyakulia Sh milioni 4 akiwashinda Maxi Nzengeli na beki Dickson Job aliokuwa akiwania nao tuzo hiyo.
Akizungumza kupitia mtandao wa klabu hiyo leo Jumanne, mchezaji huyo alisema tuzo hiyo imempa heshima kubwa na kumwongezea ari ya kuipambania timu yake katika mashindano yote ambayo wanashiriki hivi sasa.
“Nawashukuru mashabiki wa Yanga, kwa kunipigia kura, imeonesha namna imani yao ilivyo kwangu, na mimi nitahakikisha nazidi kupambana ili kuwapa mafanikio zaidi msimu huu lakini nawashukuru wachezaji wenzangu pia kwa ushirikiano wao na benchi la ufundi kwa kunipa nafasi,” alisema Aziz Ki.
Kiungo huyo ameshinda tuzo hiyo baada ya kuifungia Yanga mabao manne mwezi Oktoba katika michuano ya Ligi Kuu NBC, ikiwemo ‘hat-trick’ aliyoifunga katika mchezo dhidi ya Azam FC wiki iliyopita.
Aziz Ki kwa msimu huu ni miongoni mwa vinara wanaoongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu NBC na timu yake akifunga mabao sita sawa na Jean Baleke wa Simba.
Soka Aziz Ki awashukuru mashabiki kwa tuzo
Aziz Ki awashukuru mashabiki kwa tuzo
Read also