Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich imeendelea kukomaa katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane baada ya kuwasilisha ofa nyingine kwa mara ya pili.
Kane mwenye umri wa miaka 29 tayari amebainisha wazi kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ili kusaka changamoto kwingineko na tayari timu nne zimeingia katika mbio za kumsaka mshambuliaji huyo.
Man United ilikuwa ya kwanza ingawa baadaye ilitangaza kujitoa na kuziacha timu za PSG, Real Madrid na Bayern ambayo inaonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inampata Kane.
Vigogo wa klabu ya Bayern wanadaiwa kutofurahishwa na mwenendo wa timu yao msimu wa 2022-23 ulioisha hivi karibuni na wanaamini ipo haja ya kuiimarisha safu ya ushambuliaji na Kane anaonekana kuwa mtu sahihi katika eneo hilo.
Tangu Robert Lewandowski aihame Bayern na kujiunga na Barcelona, vigogo wa klabu hiyo ya nchini Ujerumani wanaamini walipoteza mtu muhimu katika safu ya ushambuliaji na sasa akili yao ipo kwa Kane lakini Spurs wanadaiwa kuwa wagumu kumuachia kirahisi mshambuliaji huyo.
Klabu za PSG na Real Madrid nazo zinadaiwa kufuatilia taratibu mbio za Bayern kabla ya kuamua nini cha kufanya kwani tangu zihusishwe na mpango wa kumtaka mshambuliaji huyo hakuna iliyotangaza kujitoa katika mbio hizo zaidi ya Man United.
Kimataifa Bayern yamkomalia Harry Kane
Bayern yamkomalia Harry Kane
Read also