Na mwandishi wetu
Baada ya kumsajili kiungo, Ibrahim Ajibu, timu ya Coastal Union imesema inaamini usajili wa mchezaji huyo utawasaidia kuongeza nguvu ya mapambano na kufanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu NBC.
Timu hiyo ya Tanga jana Alhamisi ilitangaza kumsajili Ajibu ambaye alimaliza mkataba wake wa mkopo kunako klabu ya Singida Fountain Gate akitokea Azam FC na kusajiliwa kama mchezaji huru.
Ofisa Habari wa Coastal, Jonathan Tito alisema Ajibu ni mchezaji mzuri ambaye wana imani naye ataisaidia timu yao kufikisha malengo waliyokusudia.
“Si mchezaji mbaya sote tumemshuhudia huko alikotoka alichokifanya na kila mmoja anafahamu ubora wake. Na sasa ametua kwetu tunaamini ataongeza nguvu na kuisaidia timu kuelekea msimu ujao utakaokuwa na ushindani mkubwa,” alisema Tito.
Mbali na Ajibu, wengine waliotangazwa katika usajili mpya wa timu hiyo ni beki wa kati kutoka Malindi ya Zanzibar, Abdallah Denis, Lucas Kikoti na Ally Kombo.
Soka Ajibu aipa matumaini Coastal
Ajibu aipa matumaini Coastal
Read also