Na mwandishi wetu
Timu ya KMC imesema bado ina matumaini ya kubaki kwenye Ligi Kuu NBC msimu ujao huku ikipigia hesabu mechi tatu walizobakiza kuwa watapambana kufa au kupona.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema licha ya kufanya vibaya katika mechi zilizopita hawapaswi kukata tamaa hadi mechi ya mwisho.
Alisema wana imani kwa maandalizi mazuri ya kikosi chao kuelekea katika mechi tatu za lama salama watashinda na kujiweka mazingira mazuri ya kubaki salama.
“Tunajua tuko katika nafasi ambayo si nzuri lakini bado hatujapoteza matumaini, tunasema haijaisha mpaka mechi ya mwisho,” alisema na kuongeza kuwa timu imejipanga kupambana.
KMC inashika nafasi ya 14 kwa pointi 26 baada ya kucheza michezo 27, kushinda sita, sare nane na kupoteza michezo 13.
Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hiyo, wameshinda mmoja na kupoteza michezo minne huku ikiwa imebakiza mechi dhidi ya Singida Big Stars, Tanzania Prisons na Mbeya City kabla ya kufungwa pazia la ligi msimu huu.
Mwenendo mbaya wa timu hiyo ulimwondosha aliyekuwa kocha wao, Thiery Hitimana na kikosi hicho kukabidhiwa Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye ana kazi ya kuhakikisha timu hiyo inabaki salama.
Soka Mechi tatu kuibakisha KMC ligi kuu
Mechi tatu kuibakisha KMC ligi kuu
Read also