Na mwandishi wetu
Timu ya Azam FC imetangaza kuachana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Kali Ongala baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa msimu mmoja.
Ongala aliyeanza kazi katika timu hiyo mwanzoni mwa msimu msimu kama kocha wa washambuliaji, baadaye alikaimu nafasi za kocha mkuu huku akiendelea na majukumu yake kabla ya jana kuelezwa ameachana na timu hiyo.
Azam imeeleza hayo leo Alhamisi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikieleza kumshukuru kwa muda wote aliokuwa nao huku ikimtakia heri katika majukumu yake mapya.
Timu hiyo yenye maskani yake Chamazi, Dar es Salaam pia ilitangaza kuachana na wachezaji wawili, mshambuliaji Ismail Aziz ‘Kader’ na kiungo Clephas Mkandala aliyedumu kwa msimu mmoja katika kikosi hicho.
Kader aliyejiunga na timu hiyo tangu msimu wa 2020-21 akitokea Prisons amekuwa akikosa nafasi kutokana na ubora wa wachezaji wanaocheza nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Mkandala aliyejiunga na kikosi hicho akitokea Dodoma Jiji.
Huo umekuwa mwendelezo wa Azam kuisafisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao baada ya juzi pia kuweka wazi kuachana na mchezaji wake mkongwe, Bruce Kangwa aliyedumu kwa miaka saba.
Wengine waliotangazwa kuachana na timu hiyo mpaka sasa ni Rodgers Kola, Kenneth Muguna na aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Dani Cadena.
Soka Azam yaachana na Kally Ongala
Azam yaachana na Kally Ongala
Read also
