Madrid, Hispania
Klabu ya Atletico Madrid imetoa taarifa ya kulaani matukio ya ushangiliaji yenye ujumbe wa ubaguzi wa rangi yaliyomlenga mchezaji wa Real Madrid, Vinicius Junior.
Tukio hilo linadaiwa kutokea kabla ya mechi baina ya timu hizo mbili, limekemewa kila kona na katika taarifa yao, Atletico wamesema kwamba watamfungia mwanachama wao yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo.
Mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Atletico wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani katika mechi hiyo ya Jumapili dhidi ya Real Madrid, walirekodiwa wakiimba nyimbo zenye ujumbe wa ubaguzi wa rangi huku vyombo vya habari vikiwa na taarifa za mashabiki waliosikika wakimshambulia mchezaji huyo wakati wote wa mechi hiyo ambayo Real iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Awali mabosi katika Ligi Kuu Hispania au La Liga waliahidi kuandika ripoti rasmi ya tukio hilo na kuifikisha katika mamlaka zinazohusika na usimamizi wa amani pamoja na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Hispania.
“Atletico Madrid inalaani tabia zisizokubalika za zomea zomea ya mashabiki wachache waliokuwa nje ya uwanja kabla ya mechi, klabu yetu wakati wote imekuwa ikijulikana kwa namna ilivyo wazi na yenye kujumuisha na kuwapa nafasi mashabiki wa mataifa, utamaduni, rangi na wa makundi tofauti ya kijamii, hivyo mashabiki wachache hawawezi kuharibu taswira nzuri ya mashabiki maelfu wa Atletico ambao wanaiunga mkono timu yao kwa heshima na mapenzi yaliyojaa hamasa.”
“Zomeazomea hii imetusababishia matatizo na kutushushia heshima na hatutakubali mtu yeyote binafsi ajifiche katika rangi zetu ili kufikisha ubaguzi wake wa rangi au wa aina yoyote, hapa Atletico hakuna msamaha dhidi ya vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Kimataifa Atletico yalaani ubaguzi kwa Vinicius Jr
Atletico yalaani ubaguzi kwa Vinicius Jr
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
