Na mwandishi wetu
Simba imefanikiwa kunyakua pointi tatu baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC iliyopigwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Simba iliandika bao lake la kwanza dakika ya 35 mfungaji akiwa ni Freddy Michael kwa pasi ya Saido Ntibazonkiza wakati bao la pili lilifungwa na Saleh Kabaraka akiitumia pasi ya Muzamir Yassin katika dakika ya 65.
Ushindi huo ambao umekuja baada ya Simba kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi zilizopita unaifanya timu hiyo kufikisha pointi 50 na kuendelea kushika nafasi ta tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 katika mechi 24.
Simba hata hivyo imezidiwa na Azam kwa mechi moja wakati Yanga inashika usukani ikiwa na pointi 62 katika mechi 24 na kwa Mtibwa mambo yanazidi kuwa magumu na wanahitaji kupambana vilivyo ili kujinasua na janga la kushuka daraja.
Timu hiyo kwa sasa ndiyo inayoburuza mkia ikiwa na pointi 17 katika mechi 24 na haitoshangaza kwa mabingwa hao wa mwaka 2000 kucheza Ligi ya Championship msmu ujao.
Simba, kabla ya mechi yake na Mtibwa ilitoka sare ya bao 1-1 na Ihefu FC kisha ikapoteza kwa mabao 2-1 mbele ya mahasimu wao Yanga kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Namungo FC.
Soka Simba yainyuka Mtibwa 2-0
Simba yainyuka Mtibwa 2-0
Read also