Manchester, England
Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag ameahidi kushughulika na Cristiano Ronaldo baada ya mchezaji huyo kutoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Tottenham jana Jumatano usiku.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, Ronaldo ambaye aliwekwa benchi aliondoka dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho kupulizwa licha ya kwamba timu yake ilitoka uwanjani na ushindi wa mabao 2-0.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 inaonekana alichukizwa kwa kitendo cha kuwekwa benchi na kutopewa nafasi ya kucheza hasa baada ya Ten Hag kuwapa nafasi Christian Eriksen na Anthony Elanga na hivyo akaamua kutoka bila ya kuwapongeza wenzake kwa ushindi.
“Nitashughulika naye kesho (leo) kwa sasa tunafurahia huu ushindi, nimemuona lakini sikuzungumza naye lolote,” alisema Ten Hag.
Katika mechi hiyo Man United ilifanya mabadiliko ya wachezaji watatu na hivyo kuwa na nafasi nyingine mbili lakini kwa Ronaldo hakuliona hilo badala yake akaamua kuondoka dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho pengine kwa kile alichoamini kuwa hakuwa na nafasi katika mechi hiyo.
Hii si mara ya kwanza Ronaldo kuingia katika mzozo kwa kile kinachoaminika kuwa ni kutokubaliana na maamuzi ya Ten Hag, Jumapili iliyopita alionekana kuchukizwa waziwazi baada ya kutolewa katika mechi dhidi ya Newcastle lakini pia aliwahi kutoka uwanjani kabla ya mpira kuisha kwenye moja ya mechi za maandalizi ya msimu wa 2022-23.
Matokeo ya mechi nyingine za EPL za Jumatano…
AFC Bournemouth 0-1 Southampton
Brentford 0- 0 Chelsea
Liverpool 1-0 West Ham
Newcastle 1-0 Everton
Man United 2-0 Tottenham
Kimataifa Ten Hag aahidi kumkabili Ronaldo
Ten Hag aahidi kumkabili Ronaldo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
