Davos, Switzerland
Mabingwa wa soka duniani Argentina wameshika usukani kwa mujibu wa viwango vya ubora vya Fifa vilivyotolewa jana Alhamisi ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka sita.
Ushindi wa Argentina katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki mwezi uliopita umetosha kuifanya nchi hiyo ishike usukani na kuibwaga Brazil ambayo imepoteza mechi ya kirafiki na Morocco kwa kufungwa mabao 2-1 na kuangukia nafasi ya tatu.
Ufaransa mabingwa wa dunia wa mwaka 2018 na ambao mwaka 2022 walifikia fainali kabla ya kufungwa na Argentina waliobeba kombe, wanashika nafasi ya pili ikiwa imetoka kushinda mechi mbili za kuwania kufuzu Euro 2024 dhidi Uholanzi na Ireland.
Ubelgiji inashika nafasi ya nne wakati England ambayo imetoka kuifunga Italia inashika nafasi ya tano, Uholanzi ya sita, Croatia ya saba na Italia ya nane, Ureno ya tisa na Hispania inashika nafasi ya 10.
Katika nchi za Afrika, Morocco inayowania kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2030 na chini za Hispania na Ureno imechomoza ikiwa katika nafasi ya 11 ikizibeba nchi za Afrika katika orodha hiyo.
Japan inaongoza timu za Asia ikiwa nafasi ya 20 wakati wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2022, Qatar wameangukia katika nafasi ya 61.
Kimataifa Argentina kinara viwango vya Fifa
Argentina kinara viwango vya Fifa
Read also