Na mwandishi wetu
Beki wa kati wa Yanga, Ibrahim Bacca ameongezewa mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2027.
Mchezaji huyo alijiunga na Yanga Januari mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar baada ya kuonesha kiwango bora kunako klabu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.
Tangu kutua Yanga, Bacca amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha kiwango bora tangu msimu uliopita, akiisaidia timu hiyo kubeba mataji ya Ligi Kuu NBC, Kombe la FA na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kupitia mtandao wake, Yanga leo Jumatano imebainisha kumalizana na mchezaji huyo kwa kuandika: “Bacca ataendelea kusalia Yanga hadi 2027.”
Kuelekea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly wikiendi hii, Bacca ndiye mchezaji aliyechaguliwa kuwa ataenziwa yaani itakuwa siku yake maalum kuthamini kazi yake na mchango anaouonesha katika klabu hiyo.
Tayari baadhi ya wachezaji kama Stephane Aziz Ki na Max Nzengeli waliwahi kuenziwa ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo wachezaji na kuthamini mchango wao.
Soka Bacca aongezewa miaka miwili Yanga
Bacca aongezewa miaka miwili Yanga
Read also